Historia ya KUWASA
KUWASA ilianzishwa mwaka 1998 chini ya Sheria ya Water Works Act, Sura ya 272 kifungu cha 3(3) iliyofutwa na Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya Mwaka 2019 (The Water Supply and Sanitation Act, 2019). KUWASA hutoa huduma za maji na usafi wa mazingira chini ya usimamizi wa EWURA, ambayo husimamia ubora wa huduma, utoaji wa leseni na uidhinishaji wa bei za huduma za maji.
Kwa mujibu wa EWURA, KUWASA ipo chini ya leseni ya Daraja la III katika Kundi B la watoa huduma za majisafi na usafi wa mazingira. KUWASA inahudumia wateja 27,391 katika kata 22, zikiwemo kata 19 za Manispaa ya Kigoma Ujiji na kata 3 za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma (Kigoma DC). KUWASA ina mtandao wa mabomba wa takribani km 420, unaowezesha upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 92 ya wakazi katika eneo la huduma.
KUWASA ina chanzo kimoja cha uzalishaji maji kilichopo eneo la Aman Beach, chenye uwezo wa kuzalisha takribani lita milioni 42 za maji kwa siku.
Kazi za Msingi za KUWASA
- Uzalishaji na usambazaji wa maji safi na salama
- Ukusanyaji na uondoaji wa maji taka
- Usimamizi wa miundombinu ya maji
- Kupanga na kutekeleza miradi ya maji
- Kulinda vyanzo vya maji
- Kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi bora ya maji
Eneo la Huduma
KUWASA inatoa huduma katika eneo la Mji wa Kigoma na vitongoji vyake. Eneo letu la huduma linajumuisha:
Eneo la Huduma
Mji wa Kigoma na maeneo yanayoizunguka
Idadi ya Watu
Zaidi ya watu 150,000
Maunganisho
Zaidi ya maunganisho 12,500
Malengo Yetu
KUWASA ina malengo yafuatayo katika kutimiza wajibu wake:
- Kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wote wa eneo la huduma
- Kuboresha ubora wa huduma za maji kwa kuhakikisha maji yanayotolewa yanakidhi viwango vya afya
- Kupunguza upotevu wa maji katika mtandao wa usambazaji
- Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ili kuhakikisha uendelevu wa huduma
- Kuboresha miundombinu ya maji taka na usafi wa mazingira